Wednesday, July 9, 2025

Jinsi ya Kuandika CV ya Kisasa Inayovutia Waajiri (2025)

  fursa       Wednesday, July 9, 2025

Watu wengi hawaitwi kwenye interview sio kwa sababu hawana elimu – ni kwa sababu CV zao hazivutii hata kidogo.

Leo nakuletea mwongozo mfupi wa kuandika CV ya kisasa inayopenya.

Mambo Muhimu kwenye CV ya 2025:

1. Jina lako na taarifa za mawasiliano – weka simu inayopatikana na barua pepe ya kitaalamu (mfano: jinalako@gmail.com).

2. Maelezo mafupi kukuhusu (Profile Summary) – maneno 2–3 kuhusu wewe, uzoefu na malengo yako.

3. Uzoefu wa kazi (kama upo) – andika kwa mpangilio wa hivi karibuni kurudi nyuma.

4. Elimu na mafunzo – weka kuanzia chuo/shule ya juu hadi ya msingi.

5. Ujuzi maalum – mfano: Microsoft Word, Photoshop, Graphic Design, Driving, Social Media, nk.

6. Referees – watu wawili wa kuaminika. Hakikisha wanajua umeweka majina yao.

⚠️ Epuka Haya:

CV yenye paragraph ndefu kama barua.

Kuweka picha ya kupendeza badala ya kitaalamu.

Kuweka taarifa za kidini, kisiasa au mapenzi (hazihitajiki!).



Join Our WhatsApp Groups to Receive Latest Jobs Updates on Your Phone

logoblog

Thanks for reading Jinsi ya Kuandika CV ya Kisasa Inayovutia Waajiri (2025)

Previous
« Prev Post